Saturday, July 23, 2011

YAO MING....ASTAAFU KUCHEZA BASKETBALL....!

                                                          YAO MING
Basketballer toka China anayechezea timu ya NBA ya Houston Rockets,Yao Ming ametangaza kujiuzu kucheza ligi ya NBA
Yao Ming inasemekana ndio mchezaji mrefu kwa sasa mwenye futi 7 na inchi 6 alikua ni mchezaji wa Houston Rockets na alifunguka kujivua gamaba hometown kwao,Shanghai akieleza kuwa majeruhi yamemfanya aamue kustaafu na mwaka 2002 alijiunga na ligi ya NBA,na kwa sasa atafaya kazi pamoja na timu yake ya Shanghai Sharks iliyopo nchini kwao na kuna uwezekano akawa Manager na ana mpango wa kufanay kazi kwenye foundation yake ya Yao Foundation

 HASHEEM THABEET MANKA - HUOSTON ROCKETS

....Kustaafu kwa Yao Ming kunakua afueni kwa Mchezaji toka Tanzania,Hasheem Thabeet Manka anayechezea timu hiyo hiyo ya Houston Rockets ku-shine coz inasemekana Hasheem alionekana ni chaguo sahihi kumrithi Yao Ming baada ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara kabla hajastaafu...!

                                           ....YAO MING FOUNDATION...

Tuesday, July 19, 2011

....LANGA AFUNGUKA....KUHUSU DRUGS...!

                                                                          LANGA
Hip-Hop Artist aliyetokea kwenye project ya Coca Cola Pop Stars,Langa Kileo amefunguka na kukiri kuwa alikua muathirika wa madawa ya kulevya na kwa sasa ameachana na hizo issue za kutumia drugs Langa mwenye diploma ya marketing,alianza kutumia drugs miaka 5 iliyopita na kumsababishia hata kupoteza kazi na kwa sasa ana miezi 4 tangu aache kutumia madawa ya kulevya....
....Akifunguka zaidi wakati anatumia drugs alifikia mpaka kuitenga familia yake na rafiki zake wa karibu na kwa sasa ametoa ngoma yake ya Boomboclat akizungumzia jinsi alivyoathirika na yuko tayari kuwa ambassador kama mfano kwa wale walioathirika ili waache....Big Up...sana kaka tunaamini utakuwa mfano mzuri wa kuigwa...!

Thursday, July 14, 2011

..WABONGO BWANA....MULIKA MWIIIIZIII...!

Hebu cheki jinsi wa Tanzania walivyokua wabunifu....hapa watu walikua wanatongozana na inaelekea hii issue ilitokea pande za Bar....Tweeeendeee...!

Njemba....Oyaa halafu baadaye unitafute...au siyo...akajibiwa na Totoz....Nikutafute saa ngapi?

Njemba....saa 4 usiku....Totoz....Wapi...?

....Njemba ikajibu...kitandani ndotoni...au sio mama...
....Na hii ni fedha halali ya Tanzania,tena kwa malipo ya shilingi elfu kumi...

Wednesday, July 13, 2011

ROSTAM AZIZ...AJIUZULU UBUNGE NA UJUMBE WA NEC.!

Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM) mkoani Tabora,Mhe Rostam AbdulRasul Aziz amejiuzulu Ubunge wa Jimbo la Igunga Inafunguliwa kuwa Rostam pia kujiuzulu Ujumbe wa NEC kwenye Chama Cha Mapinduzi aka CCM na alitoa tamko kwenye mkutano mbele ya Waandishi wa habari...

Saturday, July 9, 2011

HAPPY BIRTHDAY TO MY UNCLE HALMA MIIGO.....! i wish her long life.l

 Happy birthday to you happy birthday dear Uncle happy birthday to youuuuu.....
How old are you now.. how old are you now.....
Dah... Nakutakia maisha malefu na mungu akubariki..1

Wednesday, July 6, 2011

EMMANUEL ADEBAYOR....AONESHA JEURI YA HELA..!

                         FOOTBALLER EMMANUEL ADEBAYOR - TOGO/REAL MADRID

Mwanasoka toka Togo anayechezea timu ya Real Madrid,Emannuel Adebayor ameonesha jeuri ya fedha baada ya kuzirusha kwenye concert moja pande za Accra-Ghana
Concert ilibatizwa jina la “Ghana meets Naija” na ilikua ni mashindano ya kuimba kwa artist toka Ghana na Nigeria huku watengenezaji wa gari kali za Jaguar walikua wadhamini na walitoa magari yao kwa artist wote walioshiriki concert hiyo
Nigeria iliwakilishwa na artist Cool Temper Man,J-Martins,9Ice,Wande Coal,Naeto C na 2Face Idibia,na Ghana iliwakilishwa na artist Castro,Baby Jet Asamoah Gyan,Boogie Down Nima Generals, Swagger Boyz,Ruff N Smooth,R2Bees,D-Cryme, Guru na Power Guys,4x4

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME…!!!

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bunamwaya ya Uganda katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Kagame uliochezwa Julai 5,2011 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, sasa Simba imetangulia katika fainali hizo ambapo itamenyana na El Mereikh ya Sudan katika mechi ya nusu fainali mwishoni mwa wiki, ambapo El Mereikh ilikata tiketi hiyo baada kuifunga Ulinzi ya Kenya katika mchezo uliomalizika Julai 5,2011 kwa njia ya matuta.(Kwa hisani ya Blog ya Dina Ismail).

Friday, July 1, 2011

In Los Angeles m, gonna shoot my new Video "SPEAK WITH YOUR BODY" Feat Lil Romeo.

                                                                              AY

UJERUMANI YAKUBALI KUTOA MISAADA KWA WAPINZANI WA GADDAFI…!!!

Wanawake wakiwa katika mji wa Tripoli Libya ambayo sasa hivi iko katika mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amekutana na kiongozi wa kundi la waasi nchini Libya, mjini Berlin, kujadili usaidizi zaidi kwa waasi hao.
Serikali ya Ujerumani imeamua kutoa usaidizi wa kisiasa, kidiplomasia, na fedha katika jitihada za kuendeleza upinzani dhidi ya kiongozi wa Libya, Kanali Muammer Gaddafi.
Westerwelle amesema hili linajumuisha mali zinazomilikiwa na utawala wa Gaddafi zilizopo katika benki za Ujerumani, zinazokisiwa kufika zaidi ya euro bilioni 7.
Kiongozi wa kundi hilo la waasi, Mahmud Jibril, amesema kuwa anaheshimu uamuzi wa Ujerumani kutoshiriki katika operesheni ya shirika la kujihami NATO, kuwalinda Walibya, lakini anashukuru uungaji mkono wa nchi hiyo kwa kulitambua baraza la kitaifa la mpito, na kwa kutoa usaidizi wa aina nyingine.
Serikali ya Ujerumani hapo awali ilikubali kutoa silaha kwa mashambulio ya angani ya NATO nchini Libya.

MADONNA WANTS TO OPEN AN ORPHANAGE IN MALAWI, AFRICA…!!!

Madonna
Pop icon Madonna has made it known that she wants to open an orphanage in Malawi (a country in Africa), which is the hometown of her adopted son David and daughter Mercy.
“My short term goals are to build an orphan care center that will service and reach at least 1,000 children and I’m also actively involved in funding several orphanages that already exist,” Madonna said in a docu-series interview with ‘American Revolutionaries: The Hitmakers.’
The 52-year-old superstar had previously tried to build a Malawian school to teach 400 girls, which would have cost around $15 million. But due to unforeseen circumstances the plans fell flat in March.