Thursday, September 29, 2011

AFRIKA KUSINI KUANDAA AFRICA CUP OF NATIONS 2013


MOJA YA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA KWENYE AFCON 2013

AFRIKA Kusini watakuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 kuchukua nafasi ya Libya, ilitangaza Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).Libya imekubali kuachia wenyeji kwa sababu ya machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.
Hivyo wamategemewa kuwa wenyeji wa fainali za 2017, zilizokuwa zikitegemea kufanyika Afrika Kusini. Kubadilishana huko kwa nchi hizo mbili kulipata baraka za CAF.Afrika Kusini pia watachukua fainali za 2014 za Mataifa ya Afrika wa Wachezaji wa Ndani CHAN zilizokuwa zifanyike Libya.

Mapema mwaka huu waandaji wa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-20 yaliyokuwa yafanyike Libya waliyaondoa mashindano hayo.

Caf pia walitangaza wenyeji wengine wa mashindano yao makubwa.Namibia watakuwa wenyeji wa fainali za Mataifa ya Afrika 2014 kwa wanawake na Niger watakuwa wenyeji wa U-17 mwaka 2015.
Madagascar watakuwa wenyeji wa U17 mwaka 2017 na mwaka 2015 mashindano ya vijana U20 yatafanyika Senegal.

Wednesday, September 28, 2011

AFRIKA KUSINI....WAKATA CONDOMS ZA KICHINA....!


Mahakama ya Pretoria nchini Afrika Kusini imeizuia Serikali ya nchi kununua condoms milioni 11 toka China,wakidai kuwa ni ndogo sana kwa size
 
Wizara ya Fedha ya nchi hiyo ilikua na mkataba na kampuni iitwayo Siqamba Medical,iliyokua na mpango wa kununua condoms aina ya Phoenurse condoms toka China,na akitoa hukumu hiyo Jaji Sulet Potterill alisema condoms hizo ni ndogo sana, ni feki,na hazijathibitishwa na Shirika la Afya Duniani na hatua hiyo imekuja baada Afika Kusini kuwa na maambukizi mengi zaidi kuliko nchi yoyote duniani,kufikia watu 5.38 milioni kati ya watu milioni 50 wana virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa ukimwi

Monday, September 26, 2011

....REST IN PEACE....MAMA WANGARI MAATHAI...!

MAMA WANGARI MUTA MAATHAI (1 APR 1940-25 SEPT 2011)
Mwanaharakati wa maswala ya mazingira na haki za wanawake kutoka nchini Kenya,Mama Wangari Muta Maathai amefariki dunia Jumapili ya tarehe 25 September,Nairobi Hospital baada ya kuugua ugonjwa wa Cancer aka Saratani

MAMA WANGARI MAATHAI AKIWA NA TUZO YA NOBEL ALIYOTUNUKIWA MWAKA 2004
Mama Wangari Maathai alizaliwa tarehe 1 April,1940 na amefariki akiwa na umri wa miaka 71 Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel na kuweka historia ya kuwa mwanamke Mwafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo,Pia aliwahi kuwa mbunge wa Kenya na Waziri msaidizi katika serikali ya Mwaki Kibaki kati ya Januari 2003 hadi Novemba 2005

Tuesday, September 20, 2011

Vodacom kutoongeza mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu

KAMPUNI ya Utoaji Huduma za Simu za Mikononi ya Vodacom huenda ikajitoa katika udhamini wa Ligi Kuu ya Bara mara baada ya kukamilika kwa mkataba wake wa miaka mitano ya udhamini wa ligi hiyo.

Hali hiyo inakuja kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoridhika na mchakato wa Vodacom kuiruhusu Yanga kutumia nembo yenye rangi nyeusi badala ya nyekundu inayotumiwa na kampuni hiyo katika jezi zake.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema baada ya Vodacom kuingia mkataba kienyeji na Yanga wa kubadili rangi ya nembo, wao kama shirikisho wameiandikia kampuni hiyo ya simu na kuieleza klabu yoyote itakayobadili rangi ya nembo, hawatowajibika kwa lolote.

“Tumewaambia Vodacom, sasa klabu yoyote ikitaka kubadili rangi za nembo ya Vodacom wafanye watakavyo kwani walivyofanya na Yanga (kuingia mkataba kienyeji) si jambo la kiungwana,” alisema Tenga.

Hata hivyo katika hali ya kawaida, si jambo rahisi kwa Vodacom kukubali nembo yake ibadilishwe rangi na klabu zitakazoshiriki ligi hiyo kwani nafasi yake kibiashara inaweza kuyumba.

Mambo yote ya mkataba pia yatategemea na faida iliyopata Vodacom kutokana na ushiriki wake katika udhamini wa ligi hiyo kubwa kwa ngazi ya klabu hapa nchini.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwezi huu na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Vodacom ndiyo kampuni inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi wanaotumia simu za mikononi ikifuatiwa na kampuni nyingine
.

TP MAZEMBE WANUNUA NDEGE YAO WENYEWE, SIMBA NA YANGA VIPI?

Monday, September 12, 2011

This World Is Not My Home


  1. This world is not my home I'm just passing through
    my treasures are laid up somewhere beyond the blue
    the angels beckon me from Heaven's open door
    and I can't feel at home in this world anymore
    O Lord you know I have no friend like you
    if Heaven's not my home then Lord what will I do?
    the angels beckon me from Heaven's open door
    and I can't feel at home in this world anymore

  2. They're all expecting me and that's one thing I know
    my savior pardoned me and now I onward go
    I know He'll take me through though I am weak and poor
    and I can't feel at home in this world anymore
    O Lord you know I have no friend like you
    if Heaven's not my home then Lord what will I do?
    the angels beckon me from Heaven's open door
    and I can't feel at home in this world anymore

  3. Just up in Glory Land we'll live eternally
    the Saints on every hand are shouting victory
    their song of sweetest praise drifts back from Heaven's shore
    and I can't feel at home in this world anymore
    O Lord you know I have no friend like you
    if Heaven's not my home then Lord what will I do?
    the angels beckon me from Heaven's open door
    and I can't feel at home in this world anymore

R.I.P....TO THE HOMMIES WE LOST....IN ZANZIBAR....!


....TUKO PAMOJA NA WATANZANIA WENZETU WALIOPOTEZA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KWA KUOMBOLEZA MSIBA HUU MKUBWA WA TAIFA ULIOTOKEA VISIWANI ZANZIBAR,TUSAMEHEANE BUT NADHANI KAMA ITAKUA POA SANA TUKIKUTANA TENA KESHO KWENYE MATIN'GA MENGINE MUNGU AKIPENDA....MOURN TILL WE JOIN YOU....HOMMIES....AMEEEEN!