Baadhi ya waigizaji wakubwa wa sinema wa nchini marekani wameunganisha nguvu zao na kutengeneza filamu fupi inayotoa wito kwa dunia kutokomeza silaha za nyuklia
Muigizaji mkogwe Michael Douglas amesadia katika kutafuta waigizaji kama Roberto de Niro,Morgan Freeman na Matt Damon na Matt Damon ili washiriki katika filamu hiyo ya dakika Mbili(2)
Mastaa hao ambapo pia yumo Alex Baldwin,Danny Devitto na Martin Sheers wame mtaka Rais wa marekani Mh.Barack Obama kuweka wazi mikakati ya kupunguza na kisha kutokomeza kabisa silaha hizo, Filamu hiyo imetolewa na kujikuta ikienda sambamba na mkutano wa G8 unaofanyika kaskazini mwa Ireland.