Wednesday, June 29, 2011

JAMANI HAWA NDIO WATAWALA WETU AFRICA.....!

                                                              Mh.Robart Mugabe
Huyu ni Raisi wa Zimbabwe akiuchapa usingizi kwenye moja vikao alivyou huzuria.

JIDE APIGA KORABO NA OLIVER MTUKUDZI.....!!!!

                                             OLIVER MTUKUDZI NA LADY JAYDEE

Baada ya AY kupata shavu la kupiga korabo na wakari kutoka marekani kama nilivyo wahi kuandika siku zilizo pita sasa nyota imenza kung'ra kwa nguri wa mziki wa bongo freva Lady Jaydee. Usiku wa jumatatu ama kwa hakika ulikuwa usiku wa historia kwa mwana dada huyu na usiku wa historia kwa muzki wa tanzania kwani Jide alikuwa Studio akirekodi wimbo na Nguli la Muziki kutoka Zimbabwe au kwa Mugabe.kwa taarifa nilizo nazo wimbo utaitwa MIMI NI MIMI na utakapo kuwa tayari ataachiwa redioni.

JAMANI MIMI SINA COMMENT ZOZOTE NA HIZI KARAGOSI.


Tuesday, June 28, 2011

OLIVER MTUKUDZ.... APATA SHAVU... UNICEF..!

                                                   OLIVER MTUKUDZI - ZIMBABWE

Music legend toka Zimbabwe,Oliver Mtukudzi aka Tuku amechaguliwa kama Balozi wa UNICEF kanda ya mashariki na kusini mwa Afrika aka UNICEF Regional Goodwill Ambassador for Eastern and Southern Africa
YVONNE CHAKA CHAKA - SOUTH AFRICA

Oliver Mtukudzi atafanya kazi za UNICEF kuhamasisha vijana kuhusu HIV kwenye kanda hizo na ataungana na Mwanamuziki Maarufu toka Afrika Kusini,Yvonne Chaka Chaka ambaye anaisaidia UNICEF kupambana na Malaria.

Mwana mziki Buju Banton ahukumiwa miaka kumi Jela....!

                                         MARK MYRIE AKA BUJU BANTON

Artsit wa Reggae na Dancehall toka Jamaica Mark Myrie aka Buju Banton,amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kufadhili na kujihusisha na madawa ya kulevya mwaka 2009
Buju Banton pia ni mshindi wa tuzo za Grammy amehukumiwa nchini Marekani, na alitiwa hatiani kwa ushahidi wa video baada ya kuonekana aki-test cocaine kama ni yenyewe pande za Florida

JB Ang'ra tamasha la ZIFF atwaa tuzo ya muigizaji bora wa mwaka.

Muugizaji wa filamu Jacob Steven a.k.a JB akipokea Tuzo yake ya muugizaji bora wa mwaka kutoka kwa Profesa Martin Mhando, CO wa tamasha la kimataifa la Filamu ZIFF, Tuzo ambayo alijinyakulia kutokana na filamu yake ya senior bachelor, ambapo filamu bora ya mwaka ilikuwa Ray of Hope iliyo tengenezwa na Pilipili entertainment  chini ya muandaaji Sajni Srivastava zilizo tolewa na katika kilele cha tamasha hilo la ZIFF lililokuwa likifanyika Mji mkogwe mjini Zanzibar.

Sunday, June 12, 2011

LUPE FIASCO....AMZINGUA BARACK OBAMA...!

                                                   LUPE FIASCO

Artist Lupe Fiasco ame-make headline baada ya kumpaka Prezidaa Barack Obama wa Marekani kwa kumwitwa Rais Obama ni "the biggest terrorist" aka Gaidi mkubwa
RAIS BARACK OBAMA

Lupe Fiasco alikua alikua anafanya interview na CBS News na kufunguka kuwa yeye sio sehemu ya siasa za kimarekani coz yeye ni Rapper anayewakilisha jamii na kwa kusema Obama alitangaza kuwa Osama Bin Laden ameuwawa Afghanistan...sasa nani ni Gaidi tu...



Wednesday, June 8, 2011

MGANDA AMUUZIA NGOMA....SIR ELTON JOHN...!


Msanii toka Uganda anayeishi Uingereza,Tazz Mujagata ni mmoja kati ya wasanii wanaokuja juu sana,coz amepata offer toka kwa Sir Elton John baada ya kuvutiwa na live perfomance zake pamoja na mashairi yake mazuri na kumfanya Sir Elton John moja ya track zake
Ngoma yake iitwayo Remember,imetesa sana barani Ulaya tangu itue kitaa na ya Mpapula ilifanikiwa kushinda tuzo ya ECO media kama Best song & Video award 2011
Kwa sasa anatarajia kutia maguu Kampala kwa ajili ya kuandaa album launch yake mwakani na inasemekana kuwa anapiga sana show na ana booking ya miezi 6 ijayo kupiga show Europe na wengi wanamtabiria kuwa ni Dr Jose Chameleon mpya na tracks zake zinapatikana kwenye Facebook, Youtube na Myspace na ngoma zake za Reggeaton,Ragga na RnB zitasambaa nchini Uganda hivi karibuni na ni mmoja wa artist aliyepata shavu la ku-perform kwenye Uganda Independence day cerebrations nchini Uingereza na Marekani

NIMETUMIWA PICHA HII,NAOMBA TUITATHIMINI.


Jamani mi kila nikiitathimini picha hii sipati jibu naomba tathimini yenu ndugu zangu.

Uzi mpya wa msimu ujao.

TUNATAKA BAJETI YA KUONDOA KERO KAMA HIZI!


Wananchi wa kijiji cha Lupanga wilaya ya Ludewa mkoani Iringa wakisafiri katika usafiri wa trekta kama inavyoonekana pichani. Wananchi hao amabao wengi wao ni wakulima wameiomba serikali kuwajali katika bajeti itakayotangazwa leo huko mjini Dododma.

Monday, June 6, 2011

Mbowe atikisa nchi.


•  Dk. Slaa asema huu ni mwisho wa uvumilivu wao

HATUA ya polisi kumshikilia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, imeibua simanzi na hasira miongoni mwa viongozi, wanachama, mashabiki wa CHADEMA na watetezi wa demokrasia ya vyama vingi.
Hali hiyo ilianza kujionyesha mapema jana asubuhi jijini Dar es Salaam na katika mikoa mingine nchini baada ya taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo kusambaa.
Tofauti na ilivyo ada, eneo zima linalozunguka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam anakoshikiliwa kiongozi huyo lilikuwa limezingirwa na Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa na zana za kijeshi.
Ili kuhakikisha kuwa hali inakuwa ni ya usalama, askari hao walikuwa wakirandaranda na kuwauliza watu waliokuwa wameanza kukusanyika katika eneo hilo shughuli walizokuwa wakifanya katika maeneo hayo.
Hata hivyo askari hao hawakuweza kuwazuia vijana walioanza kukusanyika eneo hilo na kuimba nyimbo za kulaani kukamatwa kwa kiongozi huyo kabla ya askari hao kutoa tangazo la kuwatawanya.
Katika eneo la Magomeni, polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wapenzi wa CHADEMA waliokuwa wakiandamana kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi kulaani na kupinga kukamatwa kwa Mbowe.
Katika ofisi za makao makuu ya CHADEMA zilizoko Kinondoni, Katibu Mkuu wa chama hicho, Willibrod Slaa, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kulaani tukio la kukamatwa kwa Mbowe na lile la kushikiliwa kwa muda na polisi mjini Singida kwa Naibu Katibu Mkuu wao, Zitto Kabwe.
Akizungumza kwa hasira, Dk. Slaa aliwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho nchi nzima kujitokeza hadharani na kuchukua hatua za kupinga unyanyasaji na ukiukwaji wa demokrasia unaofanywa na jeshi la polisi na serikali ya CCM.
Katika tamko hilo, Dk. Slaa alisema viongozi wake hao waliokamatwa juzi, hawakukamatwa kwa mujibu wa sheria bali walikamatwa kwa mujibu wa maagizo ya kisiasa ya CCM, ambayo imeamua kutumia udikteta ili kujaribu kudhoofisha harakati za chama hicho za kuikomboa nchi.
Dk. Slaa ambaye kwa kawaida huzungumza taratibu na kwa upole, aliwataka wana CHADEMA kuacha kile alichokiita ukondoo na uvumilivu ambao wamekuwa wakiuonyesha siku zote.
Alisema tayari chama chake kimeshawasilisha malalamiko yote rasmi kwa Bunge la Uingereza (House of Commons) na vyama vya mabunge vya kimataifa kama “International Parliamentary Union” ili vichukue hatua za kidiplomasia za kukomesha unyanyasaji wanaofanyiwa wabunge wa upinzani Tanzania.
Pia alisema wameshawasilisha taarifa rasmi na yenye ushahidi wa kutosha kwa serikali ya Uingereza ya kuitaka ichukue hatua dhidi ya serikali ya Tanzania, kwani mabilioni ya pesa yaliyotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya mafunzo na programu nzima ya uboreshaji wa Jeshi la Polisi, yamefujwa huku polisi wakiwa bado hawajaelimika jinsi ya kuwatendea haki raia kwa mujibu wa sheria.
“Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) alinipigia simu akiniomba niwasihi wale vijana waondoke pale kituoni, na mimi nilimwambia sitawaambia waondoke. Sasa natangaza kuwa wafuasi wetu wote, nchi nzima sasa ni ruksa kuingia barabarani kupinga unyanyasaji huu. Viongozi waliokamatwa ni viongozi wa Watanzania.
“Asitokee mtu akatuambia tunakosa uzalendo, asitokee mtu akatuambia tunaharibu amani ya nchi. Wanaoharibu amani ya nchi ni Kikwete, CCM, na Jeshi la Polisi. Uvumilivu wetu umefika mwisho, ukondoo wetu umefika mwisho,” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na wafuasi kadhaa waliokuwa wakisikiliza tamko hilo.
Dk. Slaa alitumia muda mwingi kueleza jinsi Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoani Arusha, alivyokiuka vipengele kadhaa vya sheria kwa sababu za kisiasa, ili kujaribu kumdhalilisha na kumnyamazisha Mbowe na wabunge wa chama hicho, hasa katika kipindi hiki wanapokwenda kuipa changamoto kubwa serikali katika mkutano wa Bunge la Bajeti.
Alisisitiza kuwa, haikuwa halali kwa hakimu huyo kuamuru Mbowe akamatwe, kwani tayari alishatoa ruksa rasmi ya kimahakama ambayo iliwapa uhuru wa kuhudhuria shughuli za Bunge, wabunge wote wa chama hicho wanaokabiliwa na kesi hiyo iliyotokana na maandamano yaliyofanyika Arusha Januari 5 mwaka huu.
Katika tamko lake hilo, Dk. Slaa alieleza mambo makuu manne kuthibitisha jinsi hakimu huyo anavyoiendesha kesi hiyo kisiasa badala ya kufuata sheria.
Kwanza alisema hakimu huyo alishatoa ruksa rasmi ya kuwaruhusu Mbowe na wabunge wenzake kuendelea na shughuli za bunge, lakini kwa makusudi uamuzi wa ruksa hiyo haukurekodiwa kimaandishi katika kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo kama ilivyo kawaida.
Hawakufanya hivyo ili kujijengea uhalali wa kuja kumkamata Mbowe kama walivyofanya.
Pili, alisema hakimu huyo hadi Ijumaa iliyopita wakati anatoa amri hiyo, alikuwa bado hajatoa hati ya kuitwa kwa mdhamini wa Mbowe ili ajieleze kwanini yeye na mshtakiwa wake hawajaonekana mahakamani kama taratibu za uendeshaji wa kesi zinavyotaka.
Badala yake, alisema kuwa hakimu huyo alikimbilia kutoa amri ya kutaka Mbowe akamatwe ili kutimiza kile alichoagizwa na serikali ya CCM.
“Na mdhamini wa Mbowe hakuweza kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, sasa anakimbilia kutoa amri ya kutaka watu wakamatwe bila kutoa haki ya mdhamini kujieleza….hii si sheria, ni siasa,” alisema Dk.Slaa.
Tatu, alisema wakati hakimu huyo anaamuru Mbowe akamatwe wakili wake hakuwepo mahakamani kwa sababu alikuwa akihudhuria kesi nyingine mbele ya Jaji kutokana ratiba za kesi kugongana.
Alisema kwa sababu wakili wa mshitakiwa Mbowe alikuwa akihudhuria kesi nyingine, kesi hiyo ilipaswa kuahirishwa siku hiyo kama taratibu za kisheria zinavyotaka, lakini kwa sababu ya kutaka kuifurahisha serikali ya CCM iliyomtuma, hakimu huyo hakufanya hivyo.
Badala yake aliiendesha kesi hiyo bila wakili kuwepo na akatoa hati ya Mbowe kukamatwa.
“Kwanza kesi yetu huanza saa 3:00 asubuhi, lakini katika hali isiyo ya kawaida siku hiyo alianza kesi hiyo mapema, saa 2:30 huku akijua fika kuwa wakili wa Mbowe hayupo. Sasa mdhamini wa mshtakiwa hakuwepo na hakuwa amepewa hati ya kuitwa kujieleza, na wakili wake pia hakuwepo alikuwa mbele ya Jaji akihudhuria kesi nyingine.
“Kwa taratibu za kimahakama, alipaswa kuiahirisha kesi hiyo, lakini yeye ili aifurahishe serikali iliyomtuma, aliiendeleza na kuamuru Mbowe akamatwe,” alisema Dk. Slaa.
Nne, Dk. Slaa alisema hata yeye na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, walipokwenda wenyewe mahakamani hapo wiki iliyopita, bado hakimu huyo alionekana kuwasikiliza wanasheria wa serikali waliotaka kesi hiyo isiendelee mpaka wakamatwe na polisi, wakati kwa taratibu za kisheria hati ya kumkamata mshitakiwa huisha mara tu mshitakiwa huyo anapokuwa ndani ya mahakama.
“Lengo lao lilikuwa lazima watukamate hata ndani ya mahakama, ili mradi tu watekeleze mkakati wao wa kutaka kutukandamiza na kutudhalilisha, sisi tulikataa….tulisema polisi hamjui sheria. Baada ya kubishana nao kwa hoja za kisheria ndio wakatuacha, vinginevyo hakimu yule alikuwa tayari tukamatwe mbele yake wakati ‘arrest warrant’ inakwisha mara baada ya mshtakiwa kufika mwenyewe mahakamani,” alifafanua Dk. Slaa.
Alisisitiza kwa namna yoyote Mbowe kwa nafasi yake kama mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) hakupaswa kukamatwa wakati huu ambao anatekeleza majukumu mengi ya kibunge yanayohusiana na bajeti.
Alisema mbali na ruksa iliyokuwa imetolewa na ambayo kwa makusudi haikurekodiwa, pia hakimu alipaswa kujua kuwa kiongozi huyo alikuwa akihudhuria vikao vya kamati mbalimbali za Bunge, vikiwemo vile vya kamati za chama chake (party caucus) ambavyo vinatambuliwa na kanuni ya 110 ya Bunge.
Akizidi kuonyesha jinsi kamata kamata hiyo ya wabunge na viongozi wa upinzani ilivyo ya kisiasa badala ya kuwa ya kisheria, Dk. Slaa alisema Zitto alikamatwa juzi akiwa Singida kwa hoja kuwa alifanya kosa kuhutubia mkutano hadi saa 12:20 badala ya kumaliza saa 12:00 jioni.
Alisema huo pia ulikuwa ni uonevu wa dhahiri kwani sheria inasema wazi kuwa kwa wakati huu ambao si wa uchaguzi, mikutano ya kisiasa ruksa kufika hadi saa 12:30, kwa hiyo alifafanua kuwa Zitto hakukiuka sheria yoyote kuhutubia hadi saa 12:20.
Alisema kukamatwa kwa Mbowe na Zitto kutasababisha kikao cha kamati ya uongozi ya bunge kilichopangwa kukaa leo ili kupanga ratiba ya bunge la bajeti kisifanyike kama inavyotakiwa, kwani ni lazima mmoja wao kati ya viongozi hao wahudhurie kwa mujibu wa kanuni za Bunge.
“Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ni mjumbe wa lazima katika kikao cha kamati ya uongozi ya Bunge, asipohudhuria ni lazima ateue mwakilishi wa kuhudhuria kama kanuni zinavyotaka, sasa tutamwambia Zitto asiende, kwa sababu anayepaswa kumteua kumwakilisha yupo ndani,” alisema Dk. Slaa.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), John Heche akizungumza na wanafunzi wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu, Augustine Mwanza, pamoja na mambo mengine, alitoa onyo kwa Rais Kikwete kuwa atakuwa rais wa kwanza kuandika historia mbaya kabisa ya kusababisha machafuko katika nchi hii iwapo hataacha kulitumia Jeshi la Polisi vibaya kukandamiza wapinzani.
“Tutaendelea kuheshimu sheria za nchi na kulinda amani ya nchi hii, lakini kamwe hatutalinda uonevu, dhuluma wala unyanyasaji unaoanza kufanywa kwa kasi na Jeshi la Polisi, kwa kuwakamata wabunge na viongozi wetu wa kitaifa bila sababu za msingi. Hatuko tayari kuvumilia udikteta wa serikali ya CCM inayotaka kuigeuza nchi yetu kuwa dola ya kipolisi. Tutapigania haki bila kuogopa risasi, mabomu na virungu vya polisi.
“Tunalionya Jeshi la Polisi na CCM, Tunamuonya Rais Kikwete, tunamtaka achunge mwenendo wa serikali yake na vyombo vyake vya usalama, vinginevyo atakuwa Rais wa kwanza kuandika historia mbaya ya kusababisha machafuko katika nchi hii. BAVICHA tunaendelea kufuatilia na tuko tayari kuchukua hatua. Busara na uwezo wetu wa kulinda amani na kupigania haki, si vya kutiliwa shaka,” alisema Heche.
Wakati Heche akitoa kauli hiyo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alifika Kituo Kikuu cha Polisi na kukutana na Mbowe alilaani kitendo hicho cha polisi.
Mbali ya hilo, Profesa Lipumba alimtaka Spika wa Bunge kutoa tamko la kupinga kamatakamata hiyo ya wabunge wa upinzani ambayo imemgusa pia mbunge mmoja wa CUF.
Mbali ya Lipumba viongozi wengine wa kisiasa waliofika kituoni hapo kuonana na Mbowe ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Profesa Abdallah Safari.
Viongozi wa CHADEMA mikoani watoa tamko
Viongozi wa CHADEMA wa mikoa mbalimbali jana pia walitoa matamko ya kulaani na kupinga kukamatwa kwa Mbowe.
Mkoani Mara, Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Mwita Mwikwabe Waitara akisoma maazimio tisa ya mkutano mkuu wa dharura wa chama hicho kwa waandishi wa habari mjini Musoma jana alisema, kitendo cha polisi kumkamata Mbowe wakati wakielewa ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni hakivumiliki.
Alisema, endapo serikali na jeshi la polisi haitamwachia Mbowe mara moja, wana-CHADEMA wa mkoani Mara wataungana na mikoa mingine nchini kutumia nguvu ya umma ili kiongozi huyo aachiwe huru.
Waitara alisema kukamatwa kwa Mbowe ni kinyume cha sheria ya mwaka 1992 inayotoa kinga kwa wabunge kudhalilishwa hadharani na kusisitiza kwamba serikali inapaswa kuomba radhi kwa kitendo hicho, tena kinachofanywa kwa wabunge wa upande mmoja tu wa upinzani.
Mkoani Dodoma, viongozi wa chama hicho nao walitoa tamko hiyo jana wakitaka Mbowe aachiwe kwani vikao vya bajeti vinaanza kesho.
Tamko hilo lililosomwa na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dodoma, Steven Masawe, pamoja na kuungwa mkono na umoja wa vyuo vikuu mkoani hapa.
Kwa pamoja wameazimia kufanya maadamano ili kusitisha shughuli za Bunge kwa madai kuwa kama Mbowe hataachiwa, bunge halitakuwa na uwakilishi mzuri wa kutetea maslahi ya Watanzania.
“Inasikitisha kuona serikali ikiiacha kukamata mafisadi wanaolisababishia hasara kubwa taifa, na badala yake inakamata viongozi wema kama mwenyekiti wetu bila sababu zozote za msingi,” alisema Kalogi.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Friday, June 3, 2011

Kashfa za rushwa zaendelea kuisumbua FIFA


ZURICH, Uswisi
MAKAMPUNI makubwa mawili yanayolidhamini Shirikisho la Soka Duniani FIFA yameonyeshwa kusikitishwa na tuhuma za rushwa zinazotolewa kwa taasisi hiyo huku rais wa FIFA, Sepp Blatter akikataa kukubali kuwa Shirikisho hilo kuwa katika matatizo katika kipindi hiki.

Taarifa ya kampuni wa Coca Cola ilisema,"tuhuma hizi za rushwa kwa FIFA zinahuzunisha na pia ni mbaya kwa mchezo wa soka."Wakati Coca Cola wakitoa taarifa hiyo, kampuni la Adidas lenyewe lilisema,"migogoro na suala la rushwa yote hayo yanaumiza mchezo wa soka."

Akizungumza katika makao makuu ya FIFA mjini Zurich, raisi wa FIFA, Sepp Blatter alisema,"Soka haipo katika migogoro hivi sasa, ila soka inapitia katika kipindi kigumu hivi sasa na sisi familia ya soka ndiyo tutakao maliza kipindi hicho kigumu."

Kipindi cha hivi karibuni zimeibuka tuhuma za rushwa katika kampeni za kuwania uongozi wa FIFA, pia zimeibuka tuhuma za rushwa katika utoaji wa zabuni za kuandaa Fainali za Kombe la Dunia.

Katika siku chache zilizopita, nchi ya Qatar imeshutumiwa kwa kutoa rushwa na hivyo kufanikiwa kushinda zabuni ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia 2022, wakati raisi wa Shirikisho la Soka barani Asia,  Mohamed Bin Hammam na raisi wa CONCACAF, Jack Warner wameondolewa kataika nafasi za uongozi wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.

Kutokana na hali hiyo Bin Hammam ambaye alikuwa mpinazani wa Blatter katika kuwania nafasi ya uraisi wa FIFA alijitoa katika nafasi hiyo siku ya Jumatano na hivyo kubaki Blatter peke yake akiwania nafasi hiyo.

Makampuni ya Coca-Cola na Adidas yote yameonyesha kutofurahishwa na taarifa za rushwa ndani ya FIFA kwa sababu makampuni yote mawili ni marafiki wa FIFA, ambapo makampuni hayo hutoa fedha, vitu mbalimbali na huduma mbalimbali na zaidi hufanya katika Fainali za Kombe la Dunia ili yaweze kufahamika sehemu mbalimbali duniani kupitia matangazo.

"Tunatarajia FIFA watalishughulikia suala hili kwa hekima na busara na kuhakikisha wanalimaliza suala hili la rushwa lililojitokeza katika Shirikisho hilo,"alisema msemaji wa kampuni ya Coca Cola, Petro Kacur.

Naye msemaji wa kampuni ya Adidas alisema,"hili suala la rushwa katika FIFA ambalo hivi sasa linazungumzwa katika jamii siyo zuri kwa mchezo wa soka na pia siyo zuri kwa FIFA na washirika wake."Hata hivyo Adidas imesema itaendeleza ushirikiano wake na FIFA ambao imeanza nao miaka 30 iliyopita.

Wakati huo huo makamu wa raisi wa Shirikisho la Soka la barani Asia,Zhang Jilong amesema Mohamed bin Hammam bado ni raisi wa Shirikisho la Soka barani Asia, huku akisema FIFA haina mamlaka ya kumtoa madarakani kiongozi huyo wakati kiongozi huyo hivi sasa anafanyiwa uchunguzi wa tuhuma kwamba alinunua kura ili achaguliwe kuongoza Shirikisho hilo la Soka Duniani.

Jumapili iliyopita FIFA ilimuondoa Mohamed bin Hammam kwenye shughuli zote za michezo.

Magaidi watishia kulipua Uingereza

Mashirika
UINGEREZA imeingia katika hofu kubwa ya kushambuliwa na magaidi kufuatia tishio la Kundi la Al-Qaeda, kuwa linafanya maandalizi ya kushambulia.Habari zilizowekwa kwenye tovuti jana zilisema kundi la washirika wa Al-Qaeda, linaloaminiwa kupata mafunzo nchini Somalia, liko nchini humo kutekeleza mashambulizi.

Habari hizo zilisema mashambulizi hayo yalipangwa na  aliyekuwa Kiongozi wa Al-Qaeda, Osama Bin Laden, wakati wa uhai wake. Inasemekana wafuasi wa kundi hilo, walikuwa Somalia ambako walipata mafunzo ya juu kuhusu ugaidi na matumizi ya mabomu katika kufanya mashambulizi.

Inasemekana ndani ya kundi hilo kuna mtaalamu wa mabomu ambaye ni mwanafunzi wa zamani wa teknolojia ya habari kutoka Ladbroke Grove.

Mtaalamu huyo ametajwa kuwa ni Reza Afsharzadega, ambaye anatafutwa na maofisa wa FBI.Habari zilisema kabla ya kuuawa kwake Mei 2 mwaka huu, nje kidogo ya mji wa Abbottabad, Pakistani, bin Laden alihadi ya kuongozana na kundi hilo kwenda  Uingereza ambako wangefanya mashambulizi.

Al-Qaeda wamtangaza mrithi wa Osama



Islamabad, Pakistani
KUNDI la Al-Qaeda limemteua mwanajeshi msataafu wa Misri, Saif Al-Adel kuwa kiongozi wake wa mpito baada aliyekuwa akiliongoza, Osama bin Laden kuuawa na makachero wa Marekani Mei 2, mwaka huu.

Osama aliuawa na makachero hao wa kikosi maalumu baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Abbottabad, Kaskazini mwa Pakistani na mwili mwake kuzikwa baharini muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Kama alivyokuwa Osama, Al-Adel ni miongoni mwa viongozi wa Al-Qaeda walio kwenye orodha ya wanaosakwa na Serikali ya Marekani ama wakiwa hai au wamekufa.

Taarifa ya Al-Qaeda iliyosambazwa jana kwenye vyombo vya habari, imeeleza kuwa Al-Adel ataliongoza kundi hilo kwa muda, akisaidiwa na aliyekuwa msaidizi wa bin Laden, Ayman al-Zawahri.

‘’Yeye siyo kama ni kiongozi kamili, bali ataongoza katika kipindi hicho cha mpito hasa katika oparesheni za kijeshi," ilisema taarifa hiyo iliyonukuliwa na Shirika la Habari la

Al–Adel anatuhumiwa na Marekani kuwa ndiye aliyehusika kuzilipua kwa mabomu balozi zake za mjini Nairobi- Kenya na Dar es Salaam mwaka 1998.

Kiongozi huyo mpya wa Al-Qaeda, aliwahi kuwa mkuu wa kamati ya kijeshi ya kundi hilo baada ya kifo cha Mohammed Atef mwaka 2001.

"Katika miaka ya 1990, Al- Adel alikuwa anafanya kazi Iran," imesema taarifa hiyo.
Imeelezwa pia kuwa Al-Adel ndiye aliyekuwa mratibu wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Al-Qaeda nchini Morocco Mei, 2003.

Jeshi la Pakistani lalalamika
Jeshi la Pakistani limewasilisha  malalamiko kwa Jumuia ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (Nato), baada ya wanajeshi wake wawili kujeruhiwa katika makombora yaliyorushwa na majeshi ya jumuia hiyo juzi katika mpaka wa Afghanistani.

Katika taarifa yake jana, jeshi hilo limesema helikopta hizo za Nato zilikiuka uhuru wa anga ya Pakistani. Nato haijatoa taarifa juu ya tukio hilo.

Hata hivyo, ofisa mmoja wa jumuia hiyo, aliliambia Reuters kwa sharti la kutotajwa jina kwamba helikopta hizo ziliishambulia Pakistani baada ya kushambuliwa katika mpaka wa Afghanistani.

Maofisa wa Pakistani wamedai kuwa tukio hilo linaweza kuongeza msuguano ulioanza kujitokeza kati ya Marekani na nchi hiyo baada ya mauaji ya bin Laden.

Kilimanjaro mountain, Tanzania



The highest mountain in Africa, located in Northeast Tanzania, near the Kenya border. Born of the catastrophic movements in the Earth's crust that created the Great Rift Valley that runs from the Red Sea through Tanzania to Southern Africa, Mount Kilimanjaro is an extinct volcano, and is one of the most massive in the world'

Dar es Salaam, Tanzania

 
Dar es Salaam, Kiswahili for 'Haven of Peace', is the largest city and the political and economic capital of Tanzania. Located in a quiet bay off the Indian Ocean coast, the city has grown in economic importance to become a prosperous centr...e of the entire East African region.

It is a relatively modern city, a little more than a century old that has an old world charm. The city displays the many influences of its history. Its mixture of Arabic, Asian and European history gives a special atmosphere to surroundings, streets and life. A tour though the city to experience the true warmth and hospitality of the people of Dar es Salaam is a must!

BEN POUL AJIUNGA RASIMI NA THT.


Msanii aliekuwa chini ya producer Duke ndani ya M Lab Ben Paul, ameamua kujiunga na THT baada ya kumaliza mkataba wake na Duke, hata hivyo Ben Paul amesema pamoja na kufanya vizuri na ngoma yake ya Nikikupata na album yake kuingia sokoni, faida alioipata ni shilingi milioni moja tu.Album ya Ben paul inayoitwa MABOMA ipo sokoni tayari jipatie copy yako

Wednesday, June 1, 2011

AY kufanya nyimbo na Soulja boy.

AMBWENE YESSAYAH AKA AY 

Ambwene Yessayah aka AY aka Mzee wa Commercial amekwenda next level zaidi baada ya kufanya collabo mkali kutoka marekani,Percy Romeo Miller JR. aka Lil Romeo na D'anna Stewart,ngoma iitwayo Speak with your Body
Mbali na Lil Romeo pia kwa sasa ana mpango wa kufanya kazi na Soulja Boy,coz aliacha demo yake na baada ya Soulja Boy kuisikia collabo na Lil Romeo alizima makila kinga ya AY na kuamua kufanya nae kazi na kwa sasa AY anasubiri aletewe beats tu azifanyie kazi na mwezi ujao anatarajiwa kwenda Marekani kwa ajili ya kupiga huo mzigo pamoja na kutengeneza video ya Speak with your Body.

This blog is on test"

Huyu ndio Imani mwenyewe!