Friday, June 3, 2011

Magaidi watishia kulipua Uingereza

Mashirika
UINGEREZA imeingia katika hofu kubwa ya kushambuliwa na magaidi kufuatia tishio la Kundi la Al-Qaeda, kuwa linafanya maandalizi ya kushambulia.Habari zilizowekwa kwenye tovuti jana zilisema kundi la washirika wa Al-Qaeda, linaloaminiwa kupata mafunzo nchini Somalia, liko nchini humo kutekeleza mashambulizi.

Habari hizo zilisema mashambulizi hayo yalipangwa na  aliyekuwa Kiongozi wa Al-Qaeda, Osama Bin Laden, wakati wa uhai wake. Inasemekana wafuasi wa kundi hilo, walikuwa Somalia ambako walipata mafunzo ya juu kuhusu ugaidi na matumizi ya mabomu katika kufanya mashambulizi.

Inasemekana ndani ya kundi hilo kuna mtaalamu wa mabomu ambaye ni mwanafunzi wa zamani wa teknolojia ya habari kutoka Ladbroke Grove.

Mtaalamu huyo ametajwa kuwa ni Reza Afsharzadega, ambaye anatafutwa na maofisa wa FBI.Habari zilisema kabla ya kuuawa kwake Mei 2 mwaka huu, nje kidogo ya mji wa Abbottabad, Pakistani, bin Laden alihadi ya kuongozana na kundi hilo kwenda  Uingereza ambako wangefanya mashambulizi.

No comments:

Post a Comment