Monday, October 24, 2011

AL-SHABAB....WAANZA VITU VYAO KENYA...?!


Watu zaidi ya 13 wamejeruhiwa jijini Nairobi-Kenya na kukimbizwa Kenyatta Hospital baada ya bomu la kutupwa na mkono aka grenade kurushwa kwenye nightclub iitwayo Mwauras club leo asubuhi

Shuhuda wa tukio hilo,alifunguka kuwa kuna jamaa alikuja pande za Mwauras bar saa 9 za usiku na kuomba kuingia ndani na kurusha bomu hilo na kukimbia na polisi wa Kenya hawajufunguka ni nani muhusika,lakini kundi la waasi wa Al-Shabab toka somalia linahusishwa na tukio hilo hasa baada ya Majeshi ya Kenya kuamua kuwasaka kundi la Al-Shabab baada ya kufanya tukio la utekaji nyara wa mtalii toka Uingereza,mmoja toka Ufaransa ambaye baadaye alifariki na wafanyakazi 2 wa misaada toka Hispania waliofika Kenya na wiki iliyopita Ubalozi wa Marekani uliwatahadharisha wakenya kuwa makini na mashambulio kama hayo toka kwa kundi la Al-Shabab
 Jembe moja kutaka Al-shabab likiwa limeshika bendera yao
Hawa ni baadhi ya askali wa Al- Shabab wakiwa kazini.. Inchini Somalia

No comments:

Post a Comment