Thursday, August 25, 2011

RAIS KIKWETE....AMPIGA STOP...DAVID JAIRO!

JAKAYA MRISHO KIKWETE - TZ PRESIDENT
Rais Jakaya Kikwete ameamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw David Jairo asiendelee na kazi hadi hapo baada ya uchunguzi dhidi yake wa kuchangisha pesa ili Bajeti ya wizara yake ipite ukamilike
MIZENGO KAYANZA PETER PINDA - WAZIRI MKUU TZ
Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda alifunguka Mjengoni kuwa siku moja tu baada ya Bw Jairo kuripoti ofisini kwa shangwe,ambapo wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri,William Ngeleja walimpokea kwa vifijo,na wengine hata kusukuma gari lake hadi ofisini, Rais Jakaya kikwete amempa likizo nyingine baada ya amuzi wa kumrejesha kazini Bw Jairo kupokewa kwa husia tofauti na raia
DAVID JAIRO - KATIBU MKUU W/NISHATI NA MADINI
Jana Bunge la Tanzania lilifunguka kuundwa kwa kamati maalumu kuchunguza tuhuma hizo na inategemewa wajumbe wake watatangazwa kesho wakati wa kufunga kikao cha Bunge huku ripoti yake inategemewa kutolewa Bunge lijalo

No comments:

Post a Comment